Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliofariki Kivuko cha Mv Nyerere waongezeka

Muktasari:

  • Kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018 mpaka sasa kimefikisha watu 228 waliofariki na 41 manusura.
  • -Idadi hiyo imefikiwa leo Septemba 26,2018 baada ya mwili mmoja kuopolewa ndani ya kivuko hicho

Ukara. Idadi ya waliokufa katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, 2018 imefikia watu 228 baada ya mwili mwingine kuopolewa leo.

Watu 41 walinusurika katika ajali hiyo.

Mwili huo umeopolewa ndani ya kivuko na wazamiaji na wataalam wa uokoaji wanaoendelea na kazi ya kunyanyua na kukigeuza kivuko hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya Mv Nyerere, Isaac Kamwelwe amesema kuna uwezekano wa miili zaidi kuopolewa baada ya kivuko kunyanyuliwa na kugeuzwa.