CBA,Vodacom zafanya droo ya nne ya MPAWA

Monday July 8 2019

 

Dar es Salaam. Benki ya CBA ikishirikiana na kampuni ya Vodacom imefanya droo yake ya nne ya kuadhimisha miaka mitano ya huduma ya MPawa yenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa wateja wake.

Katika kusherehekea maadhimisho hayo, promosheni hiyo inajumuisha droo za kila wiki zilizohusu kuwekeza na kukopa na MPawa huku ukitoa washindi zaidi ya 340 walioibuka na mara mbili ya akiba zao.

Katika kuongelea kuhusu huduma hii ya Meneja Masoko wa CBA, Solomon Kawiche amegusia mambo matatu kwenye maadhimisho hayo.

Amesema Mpawa ilianza na wateja wanne tu ila hadi leo hii imefikisha wateja milioni 8.5.

Pia ameelezea jinsi MPawa ilivyofanikiwa kutoa huduma ya kuhifadhi akiba kwa kiwango cha chini cha hadi Sh1.

"Watumiaji wa MPawa hawana haja ya kutembelea matawi yetu na

Advertisement

kupitia huduma hii, wateja wetu wanapata faida kupitia akiba zao,"amesema.

Amesema MPawa imeinua hali ya maisha ya watanzania hususani wafanyabiashara wadogo.

Advertisement