Rais wa zamani Botswana akipigia debe chama cha upinzani

Muktasari:

Khama aliongoza Botswana kuanzia mwaka 2008 hadi 2018 wakati utawala wake ukikososlewa vikali na chama cha BDF ambacho sasa anakiunga mkono.

Rais wa zamani na anayekubalika nchini Boatswana, Ian Khama jana alimuunga mgombea wa upinzani- ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali enzi za utawala wake-- ikiwa ni jitihada za kumuondoa mtu aliyemrithisha cheo hicho.
Mapema mwaka huu, Khama alitangaza kuhama chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP), ambacho kimeongoza nchi hiyo tangu taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipopata uhuru mwaka 1966.
Kuondoka kwake na shutuma dhidi ya Rais Mokgweetsi Masisi kumekiingiza chama hicho katika mgogoro wa ndani kabla ya uchaguzimkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 23.
Uchaguzi huo utakuwa mtihani dhidi ya uwezo wa BDP baada ya zaidi ya miongo mitano ya kutawala nchi hiyo ambayo ina utajiri wa almasi.
Khama, mwenye miaka 66 na jenerali wa zamani na ambaye baba yake alongoza harakati za uhuru, amekuwa na tofauti kubwa na naibu wake wa zamani, Masisi baada ya kuingia ikulu Oktoba mwaka jana.
Baada ya maandamano yaliyofanyika kati mji aliokulia wa Serowe juzi Jumapili, Khama aliwaambia maelfu ya wafuasi kuwa BDP -- ambayo baba yake alishiriki kuiasisi -- imekufa.
"Chama cha baba wa taifa hili hakipo tena, kimekufa," alisema.
"Twendeni na tuipigie kura BPF na UDC," alisema Khama, akirejea chama cha Botswana Patriotic Front, chama kilichoundwa na washirika wake waliojiondoa kutoka chama tawala, na muungano wa vyama vya upinzani wa Umbrella for Democratic Change.
Alishauri wapigakura kuipigia kura UDC katika majimbo ambayo BPF haijasimamisha wagombea.
Khama pia alimpigia debe kiongozi wa UDC, Duma Boko.
"Maisha yatakuwa mazuri kama awali," kama wapigakura watamchagua Boko, alisema.
Kitendo hicho kinaonyesha mabadiliko ya ghafla tangu kipindi Khama akiwa rais (2008-2018), wakati UDC ilipokuwa mpinzani mkali wa serikali.
Katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa 2014, Boko alifikia hatua hata ya kusema kuwa alikuwa kwenye orodha ya watu waliokuwa wakisakwa na chama cha Khama ili wauawe.
Khama ni chifu wa kijadi wa Serowe, kabisa ambalo linapatikana mkoa wa kati na ambalo ni nguzo ya BDP.