Bibi wa miaka 102 apona corona Italia

Genoa. Bibi mwenye umri wa miaka 102 amepona ugonjwa wa virusi vya corona katika mji wa kaskazini mwa Italia wa Genoa baada ya kukaa hospitalini kwa siku zaidi ya 20, madaktari waliomtibu na mpwa wake waliiambia CNN.
Kiwango cha wastani cha wale ambao  wana umri mkubwa waliopatikana na corona na baadaye kufa nchini Italia kwa mujibu wa Taasisi ya Afya nchini humo ni 78.
Italica Grondona alilazwa hospitalini mwanzoni mwa Machi kwa "moyo kushindwa kufanya kazi," Sicbaldi aliiambia CNN.
"Alikuwa na dalili za virusi vya corona, kwa hivyo tulimjaribu na lakini baada ya kupatikana nao tuliendelea nae vizuri na alipona mwenyewe," Sisbaldi aliongeza.
Madaktari wanasema kesi yake iliwavutia sana kiasi kwamba waliamua kuisoma zaidi.
"Tulipata sampuli za serological, yeye ndiye mgonjwa wa kwanza tunajua ambayo inaweza kuwa imepitia  'homa ya Uhispania' tangu azaliwe mnamo 1917," Sicbaldi alielezea, akizungumzia janga la mafua la 1918/1919 ambalo liliwauwa watu wasiopungua milioni 50 ulimwenguni, kulingana na vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.
Grondona aliondoka hospitalini Machi 26 na sasa yuko katika uangalizi nyumbani kwake. "Sijui siri yake ni nini, lakini najua yeye ni mwanamke huru na wakujitegemea," mpwa wake Renato Villa Grondona aliiambia CNN.