Corona yashambulia zaidi wanene, wanaume

Vyumba vya dharura kwa ajili ya wagonjwa wa virusi duniani, madaktari na wauguzi wanaona idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake wenye dalili za ugonjwa wa Covid-19, huku unene ukionekana kuwa ni moja ya vitu vinavyozidisha tatizo hilo. Lakini watalaamu bado hawana uhakika.

Kitu kilichoanza kuonekana na kutoa taswira nchini China, ambako virusi hivyo viliibuka mwishoni mwa mwaka jana, kinaonekana kufanana na kinachoendelea katika hospitali barani Ulaya na Marekani wakati ugonjwa huo ukiendelea kusambaa.

“Wanaume wengi wana matatizo makubwa kuliko wanawake, na wagonjwa ambao wana uzito uliopindukia au walikuwa na matatizo ya afya wako hatarini,” alisema Derek Hill, Profesa wa tiba katika Chuo Kikuu London.

Takwimu za awali kutoka Kitengo cha Taifa cha Ukaguzi na Uangalizi Maalum cha Uingereza kuhusu watu waliotibiwa kwa uangalizi maalum kwa ajili ya kuchunguza virusi hivyo, zinathibitisha hilo, asilimia 73 ni wanaume na asilimia 73.4 ni wenye uzito mkubwa kupita kiasi.

Kwa mujibu wa takwimu za awali za matokeo ya wagonjwa ambao ama walipona au walifariki kwa ugonjwa wa Covid-19 katika kipindi cha kabla ya Aprili 3, wagonjwa wanene walionekana wana uwezekano mdogo wa kupona baada ya kuwa chini ya uangalizi mkubwa.

Asilimia 42.4 ya watu wenye wastani wa urefu na unene wa wastani zaidi ya 30 waliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kutibiwa kwa mafanikio, kulinganisha na asilimia 56.4 ya wale ambao BMI yao ni chini ya 25.

“Vyumba vya dharura nchini Ufaransa vimekuwa na idadi kubwa ya watu wenye uzito mkubwa au wanene,” alisema daktari wa kitengo cha uangalizi wa karibu, Matthieu Schmidt wa hospitali ya Pitie-Salpetriere jijini Paris.