Mgonjwa wa corona afariki nchini Kenya

Thursday March 26 2020

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Nairobi, Kenya. Mgonjwa wa kwanza mwenye maambukizi ya virusi vya corona nchini Kenya amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan.
Akitangaza kifo hicho leo Alhamisi Machi 26, 2020 Waziri wa Afya nchini humo, Mutahi Kagwe amesema mgonjwa huyo amefariki leo mchana.

Amesema kuwa mgonjwa huyo alikuwa mwanaume raia wa Kenya ambaye alikuwa na umri wa miaka 66.
Amesema kuwa mgonjwa huyo pia alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari
Mgonjwa huyo alirudi nchini Kenya Machi 13, 2020 akitokea Swaziland na Afrika kusini.

Leo mchana akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa huo nchini Kenya, Katibu wa Waziri wa Afya, Mercy Mwangangi alisema wagonjwa wapya watatu wameongezeka na kufikisha wagonjwa 31 wenye corona nchini humo

Advertisement