Maporomoko ya theluji yaua watu 130 Pakistan na Afghanistan

Wednesday January 15 2020

 

Islamabad, Pakistan. Watu zaidi ya 130 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya theluji katika nchi ya Pakistan na Afghanistan.

Kwa zaidi ya wiki sasa maeneo ya Pakistan na Afghanistan yamekumbwa na mafuriko na majira ya baridi kali.

Mamlaka za nchi hizo zimesema bado zinafanya jitihada kujaribu kuwaokoa watu wengine walionaswa katika theluji.

Hata hivyo, utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa hali mbaya ya hewa itaendelea kuwapo kwa siku za usoni.

Jimbo la Kashmir upande unaotawaliwa na Pakistan ndilo liliathiriwa zaidi ambako watu 62 wamepoteza maisha na wengine 10 wakiwa hawajulikani walipo.

Polisi mjini Kashmir wamesema kuwa wengi wa waathirika wa mafuriko hayo ni wanawake na watoto.

Advertisement

Nchini Afghanistan vifo 39 vimeripotiwa pamoja na uharibifu wa nyumba 300.

Pia, hali hiyo imesababisha shule kufungwa na kuzuiwa kwa matumizi ya barabara katika sehemu za Kaskazini mwa jimbo la Kashmir.

Advertisement