Pundamilia 'alibino' apatikana Masai Mara

Muktasari:

  • Kupatikana kwa mnyama huyo kumetokea siku chache baada ya pundamilia asiye wa kawaida mwenye madoa meusi kuonekana Tanzania.

Nairobi, Kenya. Pundamilia mwenye ngozi ya kipekee inayo fananana na albino ameonekana katika mbuga ya wanyama pori ya Masai Mara, Kenya.

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation la Kenya, picha za  pundamilia huyo zilimuonyesha mnyamna huyo akiwa tofauti na wanyama wengine wa jamii hiyo ambao wana mistari meupe na meusi wakati yeye hakuwa na mistahili hiyo katika eneo kubwa la mwili wake.

“Sehemu kubwa ya mwili wake haukuwa na mistari isipokuwa eneo la shingo na miguu ndiyo alikuwa na mistari meupe na meusi kama pundamilia wengine ishara inayoonyesha kama albino,” lilisisitiza gazeti hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, ripoti zinasema kwamba pundamilia huyo amepewa jina la Manie ili kumuezi muongoza watalii John Manie KiIpas ambaye ndiye alimuona kwa mara ya kwanza.

Wataalam wa wanyamapori walisema kwamba pundamilia huyo alidhaniwa kuwa na ugonjwa ambao wanyama huonyesha ulemavu fulani katika mistari yao ya mwilini.

 

Kupatikana kwa mnyama huyo kumetokea siku chache baada ya pundamilia asiye wa kawaida mwenye madoa meusi ambaye alionekana nchini Tanzania wiki moja baada ya kuondoka katika hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara.

Pundamilia huyo alipewa jina la Antony Tira ililotokana na jina la mwongoza watalii aliyemuona kwa mara ya kwanza na kuweka picha yake katika mtandao wa Facebook.

Inaelezwa kuwa pundamilia huyo ambaye alikua na miezi michache tangu azaliwe, aliondoka Kenya na wazazi wake wakati wa uhamaji wa nyumbu unaofanyika kila mwaka.

Ripoti ya jarida la Forbes ilisema kuwa picha hizo ziliwashangaza watalii ambao walipiga simu huku wapenzi wa wanyama wakitaka kumuona mnyama huyo wa ajabu.

Katika mitandao ya kijamii Gitweeta alichapisha picha ya hivi karibuni pamoja na ile ya Tira.