Rais wa zamani Burundi apinga kifungo cha maisha

Muktasari:

Rais wa zamani Burundi, Pierre Buyoya amesema leo Jumatano kuwa anapingha hukumu ya kifungo cha maisha.

Bamako, Mali. Rais wa zamani Burundi, Pierre Buyoya amesema leo Jumatano kuwa anapingha hukumu ya kifungo cha maisha jela alichohukumiwa bila ya kuwepo mahakamani, kwa kosa la kumuua mrithi wake, akisema kesi hiyo ilikuwa na msukumo wa kisiasa.

"Tunakataa hukumu kama hizi ambazo haziwezi kutubana kwa njia yoyote," alisema Buyoya, ambaye kwa sasa ni mwakilishi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Mali.