Watu watano wachomwa kisu Manchester, Uingereza

Muktasari:

  • Inadaiwa kuwa mtu mmona aliibuka ghafla na kuvamia kundi la watu kisha kuwachoma kwa kisu katika mji huo.

Manchester, Uingereza. Polisi wa kupambana na ugaidi nchini Uingereza wanachunguza tukio la mauaji ya watu watano ambao waliuawa kwa kuchomwa kisu.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa Oktoba 11, katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Uingereza katika mji wa Manchester.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo ilisema kuwa mtu ambaye aliibuka ghafla na kuvamia kundi la watu kisha kuwachoma kwa kisu katik.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu watano walijeruhiwa katika tukio hilo na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

“Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilo,” ilisisitiza taarifa hiyo.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha afisa wa polisi akimdhibiti mshukiwa huyo sakafuni.

Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la kibiashara la Arndale katikati mwa mji wa Manchester.

Mwaka 2017 mlipuaji wa kujitoa mhanga aliwaua watu 22 baada ya tamasha la muziki lilioandaliwa na mwanamuziki Ariana Grande.