Dodoma, Mbeya walia uhaba wa maji

Muktasari:

Wakati wakazi wa Jiji la Dodoma wakiiomba mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira (Duwasa) kuwasaidia kupata maji ya uhakika kila siku.

Dodoma/Mbeya. Wakati wakazi wa Jiji la Dodoma wakiiomba mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira (Duwasa) kuwasaidia kupata maji ya uhakika kila siku hata ikiwa kwa saa machache kutokana na uhaba uliopo, wakazi 20,000 wa Makao Makuu ya Ruangwa halmashauri ya wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya wamekosa huduma hiyo kwa wiki tatu sasa.

Mkazi wa Nzuguni mjini Dodoma, Jasmin Shamwepu alisema kwenye mtaa anaoishi wa Nzuguni B hawana huduma ya maji kwa miezi mitatu sasa, wamekuwa wakitegemea maji ya visima vinavyomilikiwa na watu binafsi.

Shamwepu alisema japo ana bomba la maji nyumbani kwake, lakini hajapata maji, hivyo kuiomba Duwasa kuwapatia huduma hiyo hata kama ni kwa mgao.

“Cha kushangaza kuna wenzetu wa Nzuguni C mabomba yao yanatoa maji kila siku na huko ndipo wanaouza maji kwenye matolori wanachota na kutuuzia kwa bei ya juu,” alisema.

“Hapa dumu moja la lita 20 tunanunua kati ya Sh500 na Sh1,000 na hatuna uhakika na usalama wa maji hayo,” alisema Shamwepu. Naye mkazi wa Dodoma Makulu, Doris Matula alisema wana wiki mbili sasa hawapati huduma ya maji na yanapopatikana wanauziwa kwa gharama kubwa.

Akijibu malalamiko hayo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Duwasa, Sebastian Warioba alisema shida ya maji kwenye kata ya Dodoma Makulu inatokana na kuhamishwa kwa bomba kubwa la maji ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR na

Mjini Mbeya, mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya (Mbeya -Uwwsa) Ndele Mango alililiambia Mwananchi jana kuwa sababu ya uhaba wa maji unatokana na watu wasiojulikana kuchimbua mabomba yanayosafirisha maji na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh15 milioni.