Mambo saba ziara ya Dk Bashiru Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akizungumza katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Ubungo.. Picha na Salim Shao

Dar es Salaam. Ziara ya siku mbili ya mtendaji mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally imetoa mwelekeo wa mambo saba yanayohimiza mabadiliko ya haraka ndani ya chama hicho, Serikali na kwa Watanzania licha ya mtihani mgumu katika utekelezaji wake.

Dk Bashiru aliyekuwa amebeba ujumbe wa mambo matatu ambayo ni utaifa; viapo; na uhai wa chama, alifanya ziara hiyo Jumanne na Jumatano wiki hii katika Manispaa ya Ubungo akiongozana na Kamati ya Siasa Mkoa, alitoa maelekezo mbalimbali kwa kila hoja.

Uchambuzi wa gazeti hili umebaini maeneo hayo yaliyobeba ziara hiyo ambayo baadhi huenda yakawa changamoto katika utekelezaji wake, ikiwamo wimbi la baadhi ya viongozi wa mashina kujiuzulu ili kugombea nafasi za uongozi kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24.

Mmoja kati ya makada wa chama hicho mkoani Morogoro, Robert Fransis alisema taadhari ya Dk Bashiru itaepusha mpasuko ndani ya chama licha ya ugumu wa kukubaliana na mazingira ya kutochukua fomu za kugombea, akisema hali huwa mbaya zaidi ngazi ya kamati ya siasa kuliko viongozi wa mashina.

“Msiwanyime fomu wakimbizi lakini wakichukua fomu watakuja kwenye taratibu za uchaguzi, mimi ni katibu wa kusimamia kanuni zilizopitishwa. Tunayo kanuni yetu, mtu mmoja cheo kimoja. Hii itafanya kazi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao,” alisema.

Kwa undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi Jumapili 1 septemba, 2019