VIDEO: NEC kuwashughulikia wasimamizi watakaovuruga uchaguzi wa ubunge, udiwani

NEC kuwashughulikia wasimamizi watakaovuruga uchaguzi wa ubunge, udiwani

Muktasari:

Makamu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mbarouk Salim Mbarouk amesema hawatasita kumchukulia hatua msimamizi wa uchaguzi atakayefanya vitendo vitakavyoharibu uchaguzi wa ubunge na udiwani.

Amesema atakayesababisha matokeo ya uchaguzi kutenguliwa na mahakama baada ya uchaguzi kwa kutozingatia maelekezo ya NEC, jambo litakalosababisha uchaguzi kurudiwa, atatakiwa kulipa fidia ya hasara hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 89 B ya sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 na kifungu cha 88A cha sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura 292.

Ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 17, 2020 katika kikao kilichojumuisha waratibu na wasimamizi wa uchaguzi mikoa ya kanda ya Kaskazini ambayo ni Kilimanjaro, Arusha Manyara na Tanga.

Amesema ni matarajio ya NEC kuwa wasimamizi hao watasimama vyema kwenye nafasi zao ili kuleta matokeo chanya katika uchaguzi mkuu.