Usajili kwa alama za vidole unavyotishia kampuni za simu

Mpaka mwishoni mwa mwaka huu, kila mmiliki wa simu ya mkononi anatakiwa kusajili laini yake kwa alama za vidole, Serikali imeagiza.

Kutofanya hivyo, itamaanisha kutoweza kupiga wala kupokea simu. Vilevile, muhusika hatoweza kutuma wala kupokea ujumbe mfupi wa maneno.

Wakati takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zikionyesha kuwapo kwa zaidi ya watumiaji milioni 43 wa simu za mkononi waliosajiliwa, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) inasema imekwishatoa namba za vitambulisho kwa watu milioni 15 mpaka sasa.

Kwenye mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Septemba, mwenyekiti wa bodi ya Vodacom, Ali Mufuruki alionyesha wasiwasi na kusema huenda wateja wengi wasifanikiwe kusajili laini zao kwa wakati hivyo kuiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza muda.

“Mpaka Septemba 20, wateja milioni mbili tu kati ya milioni 14 wa Vodacom walikuwa wamesajiliwa kwa alama za vidole. Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza muda,” alisema.

Kwa undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi Alhamis ya Octoba 03, 2019.