Sheikh Kipozeo: Magufuli I love you so much

Muktasari:

  • Shekh Hilal Shaweji maarufu  Shekh Kipozeo amesema ana kila sababu ya Kumuambia Rais wa Tanzania kuwa anampenda sana kutokana na maendeleo anayoyafanya.

Dar es Salaam. Shekh Hilal Shaweji maarufu  Shekh Kipozeo amemuambia rais wa Tanzania, John Magufuli anampenda sana kutokana na juhudi anazozifanya.

Shekh Kipozeo ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21, 2019 katika hafla ya Shirika la SimuTanzania (TTCL) kutoa gawio kwa Serikali  inayokwenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.

Amesema wakati Magufuli akiingia madarakani kulikuwa hakuna ndege hata moja lakini hadi hivi sasa zimefika nane hivyo ana kila sababu ya kumuambia nampenda.

“I love you so much, ilikuwa ni ndoto yangu kukutana na wewe ili nikuambie maneno haya leo niko mbele yako naomba nikuambie hivyo.”

“Nilipata nafasi ya kuzionja ndege hizo, nilipanda kwenda Mwanza na kurudi na nikapanda kwenda Burundi, Mwenyezi Mungu akubariki  sana mzee wetu pamoja na viongozi wetu,” amesema Kipozeo na kumaliza na kw akuomba dua.

Katika hafla hiyo ya upokeaji wa gawio viongozi mbalimba wa serikali wamehudhuria akiwemo Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally,  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Maria Sasabo, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katibu mkuu wa wizara ya Fedha Dotto James,