Rais Magufuli afanya uteuzi mwenyekiti baraza la maadili

Tuesday August 13 2019

 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Jaji mstaafu Ibrahim Mipawa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Agosti 13,2019  na Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imesema Jaji Mipawa anachukua nafasi Jaji mstaafu Januari Msofe ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Taarifa hiyo imesema uteuzi wa Jaji Mipawa umeanza Agosti,7 mwaka 2019.

Advertisement