Diamond, Nandy, Ray Vanny, Babu Tale washinda tuzo Marekani

Sunday October 20 2019

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Diamond Platnumz, Nandy, Ray Vanny na mtangazaji Lily Ommy pamoja na Babu Tale wameshinda tuzo kwa vipengele tofauti African Entertainment Awards USA (AEAUSA) nchini Marekani usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Oktoba 20, 2019.
Diamond Plutnumz ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) katika kipengele cha ‘Best Collaboration Award’ kupitia wimbo wake wa Baila.
Katika kipengele hicho Diamond ameshinda na mwenzie @miribenari ambaye ndiye aliyemshirikisha kwenye wimbo huo, Hata hivyo Diamond hakuwepo katika sherehe hizo na tuzo yake ilipokelewa na Miri Ben-Ari.
Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni Rayvanny na Nandy katika vipengele vya Best Male/Female in East, South and North Africa.
Pia Mtangazaji wa kituo cha Times FM, Lil Ommy naye ameshinda tuzo ya ‘Best Host’, Huku Babu Tale akichukua tuzo ya Meneja bora wa wasanii barani Afrika.

Advertisement