Mgonjwa mwingine wa corona abainika Zanzibar

Muktasari:

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imethibitisha mgonjwa mmoja wa virusi vya corona visiwani humo hivyo kufanya idadi kuwa watatu huku kwa Tanzania bara wakiwa 11 na kufanya jumla kufikia 14. 

Zanzibar. Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid amesema mgonjwa wa virusi vya corona amebainika visiwani humo ambaye ni rai wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 28,2020, Waziri Rashid amesema mgonjwa huyo mwenye umri wa miaka 57 ni mwanamke raia wa Tanzania aliyetoka safarini nchini Uingereza.
Amesema mwanamke huyo anafanya idadi ya wagonjwa wa corona visiwani humo kufikia watatu huku Tanzania Bara wakiwa 11 hivyo kufikisha 14 kwa Tanzania nzima.