Breaking News

Profesa Lipumba kuwapiga chini wanasiasa cheo cha U - DC

Sunday October 18 2020

 

By Janeth Joseph, Mwananchi

Nanyumbu. Mgombea urais wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema endapo akiingia madarakani atahakikisha anafanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wenye vigezo vya kusimamia maendeleo ya wananchi na si wanasiasa.

Amesema wakuu  wa Wilaya atakaowateua ni wale ambao watakuwa  watumishi wa serikali kwa lengo la  kuondoa changamoto zinazojitokeza baina ya wananchi na viongozi hao.

Aidha, amesema mfumo wa uteuzi wa wakuu wa wilaya kwa sasa unawalenga wanasiasa ambao mara zote huchangia kuwapo kwa migogoro mingi na wananchi.

 

Na baadhi yao hutumia vyeo hivyo kwatesa wananchi kwa kuwaweka mahabusu kwa saa 24 bila sababu za msingi.

Profesa Lipumba ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 18, 2020 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mangaka Jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara.

Advertisement

“Wananchi wa Nanyumbu naomba mnichague ili tukapate katiba yenye misingi ya demokrasia itakayolinda haki za binadamu na kuweka utaratibu wa wakuu wa wilaya watateuliwaje.”

“Nitahakikisha kwenye katiba hiyo lazima wakuu wote wa wilaya wanapoteuliwa wanakuwa na vigezo vyote vya utumishi wa serikali na sio wanasiasa,” alisema.

Profesa Lipumba alisema watumishi wa umma watakuwa na uwezo wa kuzingatia, kusimamia na kuendeleza maendeleo katika maeneo yao. “Tunahitaji serikali ya umoja wa Kitaifa ili tupate katiba yenye misingi ya demokrasia na kulinda haki za watu na kulinda mali za wananchi,” alisema.

Advertisement