Ajali yaua 18 Mkuranga, 15 wajeruhiwa

Wednesday April 15 2020
pic ajali

Dar es Salaam. Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Aprili 15, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.

“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amesema Lyanga.

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.

Advertisement