Ajira serikalini mpaka Kitambulisho cha Taifa

Dar es Salaam. Unataka kuomba kazi seri-kalini? Hakikisha una Kitambulisho cha Taifa.Sekretarieti ya Ajira imetangaza kuwa hadi mwisho wa mwezi huu, watu wote wanaoomba ajira serikalini lazima wawe na Kitambulisho cha Taifa ili kutimiza vigezo. Tangazo hilo limewashtua baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu na vyama vya wafanyakazi waliozungumza na gazeti la The Citizen walioonyesha wasiwasi wao kwamba watu wengi watafungiwa nje kwa kuwa tarehe ya mwisho ipo karibu.

 Kupitia tovuti ya http://portal.ajira.go.tz/ sekretarieti hiyo imetangaza kuwa wanao-tafuta ajira serikalini ni muhimu watafute kwanza namba za vitambulisho vya Taifa (NIN) kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida).

Simu iliyopigwa na mwandishi wa habari hizi katika dawati la msaada (huduma kwa wateja) kupitia namba +255 784 398 259 inayopatikana http://portal.ajira.go.tz ilit-hibitisha tangazo hilo. Kwa mujibu wa mtoa huduma huyo, mfumo huo bado haujaanza kutumika bali tangazo hilo lililenga kuwaandaa waombaji kutafuta vitambulisho hivyo ifikapo Novem-ba vitakaponza rasmi kutumika kwa kazi hiyo wasisumbuke. Hata hivyo, mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu alikosoa mab-adiliko hayo akisema yamelenga kuwazuia watu wanaotakiwa kuajiriwa na Serikali kwa sababu tarehe ya mwisho iko karibu mno kwao kutafuta vitambulisho.

“Kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika mfumo wa ajira, unataarifiwa kuwa kuanzia mwisho wa Septemba, 2019 mtat-akiwa kuwa na namba za vitambulisho vya Taifa kukamilisha uombaji,” imesomeka sehemu ya tangazo hilo. Tangu Mei mwaka huu, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza usajili wa laini za simu kwa njia ya biometriki kuweka kitambulisho cha Taifa kama kigezo muhimu.

Hadi Septemba mwaka huu, ni watumiaji wa simu 5.2 milioni, sawa na asilimia 12 ndi-yo waliosajiliwa. Malalamiko yamekuwa yakitolewa juu ya ucheleweshwaji wa vitambulisho vya Taifa kupitia Nida, hali inayohofiwa kuwakosesha watu huduma muhimu baada ya tarehe za mwisho kupita. Mhitimu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA), Glory Kailima alizungumzia hatua ya sasa ya Sekretarieti ya Ajira akisema wahitimu wengi wa vyuo watakosa fursa za ajira. “Muda uliowekwa na Serikali kwa wata-futaji wa ajira siyo sahihi. Angalau wange-kwenda sawa na usajili wa laini za simu unaoishia Desemba,” alisema.

Akizungumza na The Citizen Alhamisi iliyopita, mkuu wa mawasiliano wa Nida, Thomas William alisema mamlaka hiyo ime-shasajili watu 15 milioni wenye uwezo wa huduma za kitaifa kupitia vitambulisho au kwa namba za utambulisho. “Kwa wakati huu ambao zoezi likiende-lea, siyo lazima kuwa na kitambulisho.

 Hata namba tu itasaidia,” alisisitiza. Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafan-yakazi (Tucta), Tumaini Nyamhokya alise-ma licha ya kuwa Kitambulisho cha Taifa ni nyenzo muhimu, lakini Serikali inapaswa kujua watu wake, siyo wengi walioweza kuvipata, wengine wamesubiri hadi miezi sita bila kuvipata.

 “Muda uliowekwa ni mfupi mno kukamili-sha na kupata vitambulisho,” alisema. David Rimisho, ambaye alihitimu mwa-ka jana kozi ya ustawi wa jamii alisema “tunajua umuhimu wa vitambulisho vya Taifa, lakini waangalie muda uliowekwa vinginevyo idadi kubwa ya watu wanakosa nafasi,” alisema.

Maeneo mengine ambayo Kitambulisho cha Taifa ni lazima

Kusajili kampuni: Kwa sasa huwezi kusajili kampuni katika Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) bila kuwa na kitambulisho hicho

 Pasipoti : TaifaIli Mtanzania apate hati ya kusafiria ni lazima awe na Kitambulisho cha Taifa au namba yake.

Leseni ya udereva : Huwezi kupata leseni ya udereva kama huna Kitambulisho cha Taifa au namba.

Kusajili laini za simu:  Pia ukitaka kusajili laini ya simu kitambulisho hicho ni muhimu kuwa nacho vinginevyo laini yako haiwezi kusajiliwa

Umiliki wa Ardhi :Ili kumiliki ardhi utatakiwa uwe na leseni ya udereva au hati ya kusafiria, vyote hivyo pia huwezi kuvipata bila ya kuwa na Kitambulisho cha Taifa

Ajira sekta Binafsi: Baadhi ya kampuni nchini sasa zinaajiri wafanyakazi wapya kwa sharti la kuwa na Kitambulisho cha TaifaIli