Bajeti yapendekeza kufutwa kwa tozo tano

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiingia bungeni huku akionyesha begi lililokuwa hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, kwa ajili ya kuiwasilisha jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Serikali imeliomba Bunge kufuta baadhi ya tozo zilizopo kwenye biashara ya samaki ili kukuza sekta hiyo kuanzia Julai Mosi.


Dae es Salaam.  Serikali imependekeza kufuta tozo ya ukaguzi wa maduka ya vyakula na usajili wa maduka ya dawa za mifugo.

Wamiliki wa maduka ya vyakula walikuwa wanalipa Sh50,000 wakati  waliotaka kusajili maduka ya dawa za rejareja za mifugo walitozwa kati ya Sh50,000 hadi Sh100,000.

Mapendekezo hayo yametolewa leo, Juni 13 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa anawasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 uliofanyika jijini Dodoma.

 “Pia, naomba Bunge liridhie kufutwa kwa tozo ya ukaguzi wa viwanda vya samaki nchini ambayo ni kati ya Sh200,000 hadi Sh250,000 na tozo ya leseni ya mwaka ya biashara ya samaki iliyokuwa kati ya Sh50,000 hadi Sh300,000,” amesema Dk Mpango.