Burkina Faso yatangaza siku za maombolezo

Saturday November 9 2019

 

Ouagadougou. Kufuatia shambulio la kigaidi lililoua watu 38 nchini Burkina Faso, Serikali ya nchi hiyo imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Watu wasiofahamika wanaoaminika ni kundi cha kijihadi, wameshambulia mabasi matatu wafanyakazi wa kampuni ya kuchimba madini na kuua watu hao huku wengine 63 wakijeruhiwa.

Akihutubia wananchi kupitia televisheni, Rais wa nchi hiyo, Roch Marc Christian Kabore amesema shambulio hilo ni pigo kwa Taifa na kuwataka wananchi kuungana kuhakikisha wanayashinda makundi ya kijihadi.

Kwa miezi kadhaa sasa nchi ya Burkina Faso inashuhudia mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wanajeshi na raia kwenye maeneo ya Kaskazini ambako inapakana na nchi za Nigeria, Niger na Mali.

Rais wa Burkina Faso amelitaja shambulio hilo kama uhalifu wa hali ya juu, lililotekelezwa na watu wenye silaha wasiojulikana.

"Vitendo hivi viovu vinakumbusha enzi zilizopita, ambavyo vinalenga kuzua hofu kwa wananchi na kuhatarisha demokrasia.

Advertisement

 

Advertisement