Dk Bashiru: Vyama vya upinzani vitakufa kimoja baada ya kingine

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt,Bashiru Ali akizungumza na viongozi mbali mbali wa Chama hicho mkoa wa kaskazini Unguja.bPicha na Muhammed Khamis

Muktasari:

  • Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema vyama vya upinzani nchini Tanzania vitaendelea kufa kimoja baada ya kingine kwa kuwa vinashindwa kufanya siasa vikubalike kwa wananchi.

Unguja. Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema vyama vya upinzani nchini Tanzania vitaendelea kufa kimoja baada ya kingine kwa kuwa vinashindwa kufanya siasa vikubalike kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema baadhi ya vyama hivyo huibuka wakati wa uchaguzi jambo linalovifanya vishindwe kukubalika.

Amesema kwa msingi huo, CCM kitaendelea kuimarika zaidi, akibainisha kuwa udhaifu wa vyama vingi vya upinzani ni kukosa watu sahihi wa kuviongoza.

“Adui wa vyama vya upinzani yupo ndani mwao wenyewe wasitafute mchawi lazima wakubali kubadilika,” amesema Dk Bashiru.