Dk Bashiru awapa kadi wanachama wapya 905 CCM

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk Bashiru Ally akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa chama hicho mkoa wa kusini Pemba. Picha na Muhamme Khamis

Muktasari:

Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewakabidhi kadi wanachama wapya 905 wa chama hicho Mkoa wa Kusini Pemba.

Pemba. Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewakabidhi kadi wanachama wapya 905 wa chama hicho Mkoa wa Kusini Pemba.

Baada ya kuwakabidhi kadi amewataka wasome masuala ya itikadi kwa miezi mitatu wajifunze mwenendo wa chama hicho, kuwa wazalendo.

Dk Bashiru aliyepo Pemba kwa ziara ya siku tatu amekabidhi kadi hizo leo Jumanne Desemba 3, 2019 akibainisha kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kuna haja ya kuongeza wanachama wapya.

Amewataka kushirikiana na wasiokuwa wanachama wa chama hicho ili nao wajiunge nacho.