Gharama leseni ya udereva, usajili magari yapanda

Muktasari:

Serikali imependekeza kurekebisha Sura ya 160 ya Sheria ya Usalama Barabarani ili kuongeza muda wa leseni za udereva na kupandisha malipo yake, kuongeza gharama za usajili wa magari, pikipiki na bajaji.


Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imependekeza kuongeza muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi mitano tozo zake kupanda kutoka Sh40,000  ya sasa hadi Sh70,000.

Mapendekezo hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa anasoma bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20 leo Alhmaisi, Juni 13, 2019.

Aidha Waziri Mpango amendekeza kuongeza tozo ya usajili wa magari kutoka Sh10,000 hadi Sh50,000 na pikipiki za matairi matatu (bajaji) kutoka Sh10,000 hadi Sh30,000, na pikipiki za kawaida kutoka Sh10,000 hadi Sh20,000.

Waziri huyo amesema lengo la mapendekezo hayo ni kupunguza gharama za kuchapisha leseni kwa miaka mitatu kwani leseni hizo zinaweza kudumu hata zaidi ya miaka mitano.