Hillary Clinton asema ni aibu kutochapisha ripoti ya Urusi

Muktasari:

Ataka kila mtu anayepiga kura katika nchi hiyo anastahili kuona ripoti hiyo kabla ya uchaguzi.

Washington, Marekani. Hillary Clinton amesema kuwa ni aibu kwa Serikali kushindwa kuchapisha ripoti tuhuma zinazomkabili kiongozi wa nchi hiyo, Donald Trump.

Hillary ambaye pia aliwahi kugombea nafasi ya urais wa nchi hiyo, alisema “kila mtu anayepiga kura katika nchi hiyo anastahili kuona ripoti hiyo kabla ya uchaguzi.

“Haiwezekani na ni aibu kwamba Serikali haijachapisha ripoti juu ya madai ya kuingiliwa kwa Urusi katika siasa za Marekani,” alisema Hillary.

Hillary ambaye ni mke wa zamani wa Rais wa Marekani, Bill Clinton, alisema hayo leo Jumanne Novemba 12 wakati alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC.

Kwa sasa ripoti hiyo ambayo imepata kibali rasmi cha usalama haitatolewa hadi siku ya kupigiwa kura inayotarajiwa kufanywa Desemba 12, mwaka huu.

Trump anatuhumiwa kumpigia simu Rais wa Urusi, Vladimir Putin na kuomba msaada wa kumchafua mpinzani wake, Joe Biden ili kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hata hivyo, Rais Putin amekana tuhuma hizo.

Kutokana na tuhuma hizo, Spika wa Bunge, Nancy Pelosi alitangaza mchakato wa kumng’oa Rais huyo na kuanzisha uchunguzi dhidi yake shughuli za Urusi katika demokrasia ya Marekani.    

Hillary ambaye alikuwa Uingereza alisema ripoti hiyo inapaswa kuwa wazi kwa kila Mmarekani na haipaswi kufichwa.

Hillary alisema “kwa hakika watu ambao wanakaribia kupiga kura katika mwezi mmoja wanastahili kujua ni nini hasa kipo katika ripoti na si kubashiri. Lazima liwe jambo la wasiwasi, vinginevyo kwa nini halitafichuliwa hadharani?"