Mfumo mpya wa Huawei kuzikomboa taasisi zinazotumia mifumo ya Tehema

Sunday November 17 2019

 

By Ephrahimu Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Kampuni ya Huawei Cloud imeboresha mfumo wake wa huduma kwa kuanzisha uitwao Kunpeng ECS (Elastic Cloud Server).

Mfumo huo unatajwa kuwa utaongeza ufanisi wa huduma, unafuu na uharaka.

Mfumo huo wa kompyuta unatarajiwa kuanza kupatikana katika soko la Afrika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

Jambo hilo linaelezewa kuwa huenda likawa neema kwa taasisi za umma na binafsi zinazotumia mifumo ya Tehama katika shughuli zake.

“Kwa dhati tumekusudia kutoa huduma za kompyuta huku tukifanya ubunifu wa hali ya juu ili kusaidia taasisi za umma, sekta binafsi na kampuni mbalimbali kuweza kutimiza malengo yao ya kukua zaidi,” alisema Rais wa Huawei Rui Houwei.

Houwei amesema mfumo huo mpya utakuwa na kasi zaidi kwa asilimia 15 na ufanisi wake ni asilimia 30 zaidi ukilinganishwa na mifumo mingine iliyopo sokoni.

Advertisement

 

Advertisement