Jinsi moto ulivyomfuata aliyekimbilia juu ya mti

Monday August 19 2019

 

By Juma Mtanda, Morogoro [email protected]

Morogoro. Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Gilbert Mvungi amesema mmoja wa waliofariki dunia katika ajali ya moto ya lori la mafuta Agosti 10, alipanda juu ya mti kujiokoa.

Alisema baada ya lori hilo kupinduka, mtu huyo alikuwa mmoja wa waliokuwa wakikinga mafuta hayo katika madumu na baada ya moto kulipuka alikimbia na akiwa na dumu lake na alipoona moto umekuwa mkali alipanda juu ya mti.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10 katika Mtaa wa Itingi, Msamvu, Barabara ya Morogoro - Dar es Salaam baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Akizungumza na Mwananchi jana Mvungi alisema, “baada ya moto kuanza mtu huyo alikimbia na dumu lake na wakati huo mafuta yakawa yanadondoka chini. Alipofika sehemu ambayo ni salama aliweka dumu chini na kupanda juu ya mti.”

Alisema wakati akikimbia, moto ulikuwa ukifuata matone ya mafuta na hata alipopanda kwenye mti ulimfuata.

“Baadaye akashuka chini ambako moto umeanzia na akawa hana namna nyingine,” alisema Mvungi.

Advertisement

Kwa taarifa zaidi usikose Gazeti la mwananchi leo Agosti 19, 2019.

Advertisement