Kim Jong Un asimamia tena jaribio la kombora

Muktasari:

Kim Jong alisimamia tukio hilowakati majeshi ya nchi hiyo yalipofanya majaribio ya kifaa hicho kipya lenye lengo la kuitisha Korea Kusini.

Korea Kaskazini. Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kwa mara nyingine amesimamia jaribio la kombora jipya lilotengezezwa na nchi hiyo.

Shirika la habari la nchi hiyo, liliripoti kuwa Kim Jong alisimamia tukio hilo jana Jumamosi Agosti 24 wakati majeshi ya nchi hiyo yalipofanya majaribio ya kifaa hicho kipya yenye lengo la  kuitisha Korea Kusini.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya kiasa wanasema kuwa hatua hiyo itasambaratisha juhudi za kuanzishwa tena kwa mashauriano ya kusitisha matumizi ya kinyuklia baina ya nchi hizo mbili.

Taarifa ya Jeshi la Korea Kusini imesema kuwa Korea Kaskazini imezindua kile kilichoonekana kuwa ni makombora mawili ya masafa mafupi siku ya Jumamosi lakini shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini limesema kuwa roketi kubwa zaidi imefanyiwa majaribio.

Uzinduzi huo ni sehemu ya majaribio kadhaa ambayo yanaendelea kufanywa na nchi ya Korea Kaskazini yenye lengo la kuitisha Korea Kusini.

Korea Kaskazini imefikia hatua hiyo ikiwa ni juhudi za kupinga shughuli za kijeshi za ushirikiano kati ya Marekani na Korea Kusini.