VIDEO: Rais Magufuli apiga simu kwenye mkutano wa wasanii Tanzania

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Magufuli ampigia simu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa na kuzungumza na kiongozi wa wasanii akieleza anafuatilia kongamano lao.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amempigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kueleza kuwa anasikiliza kinachoendelea kwenye kongamano la sanaa la Mwalimu Nyerere.

Rais Magufuli alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo linalofanyika leo Ijumaa Novemba 15, 2019 ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam lakini amewakilishwa na Majaliwa ndipo alipopiga simu kueleza anasikiliza kinachoendelea.

Simu hiyo ilipelekwa moja kwa moja kwa rais wa Shirikisho la Muziki Ado Novemba aliyekuwa akisoma risala kwa niaba ya wasanii.

“Nakusikiliza hotuba yako wewe soma yote nayafuatilia na maagizo yenu nimempa Waziri Mkuu atawapa, nawapenda sana, endelea kusoma nasikiliza,” amesikika Rais Magufuli huku akishangiliwa na wasanii waliojitokeza katika kongamano hilo