VIDEO: Magufuli aeleza Pinda anavyomsaidia kuongoza

Wednesday October 9 2019

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ni kati ya viongozi wastaafu wanaomsaidia kuongoza nchi.

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 9, 2019 mkoani Katavi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa kilomita 76.6.

“Leo ilitakiwa awepo hapa Mzee Pinda ananisaidia sana katika kazi, yule baba ana moyo wa kipekee.”

“Ni mtu mwema sana  na ndio maana nimemchagua kuwa  mjumbe wa  kamati kuu. Ananisaidia kuongoza nchi, chama katika mambo mbalimbali kwa sababu ni mtu mmoja mstaarabu sana,”

Ameongeza, “Na ndio maana nimemtuma China akaniwakilishe katika maadhimisho ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere. Niliona  sina mwingine wa kumtuma atakayeniwakilisha vizuri nikasema Mizengo Pinda ndio aende, ni baba mwenye moyo wa tofauti.”

Advertisement