Magufuli asisitiza Magereza kuanzisha miradi, kuwatumia wafungwa

Muktasari:

Rais  wa Tanzania, John Magufuli amelitaka Jeshi la Magereza kuanzisha na kutekeleza miradi ya uchumi na uzalishaji mali itakayowajengea  uwezo wa kujitegemea.

Mwanza. Rais  wa Tanzania, John Magufuli amelitaka Jeshi la Magereza kuanzisha na kutekeleza miradi ya uchumi na uzalishaji mali itakayowajengea  uwezo wa kujitegemea.

Akifungua mkutano wa majadiliano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) jijini Mwanza leo Alhamisi Desemba 12, 2019, Rais Magufuli ameliagiza Jeshi la Magereza kuwatumia wafungwa kuzalisha mali.

“Wafungwa watumike kuzalisha ili kuiwezesha Magereza kujitosheleza katika mahitaji na kubakiwa na ziada,” amesema Magufuli.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ameagiza kila gereza nchini kuwa na mradi ya kilimo, ufugaji na mafunzo maalum ya kuwajengea vijana uwezo wa uzalishaji na kujiajiri kulingana na mazingira ya kijiografia na shughuli za kiuchumi kwa eneo husika.