Majaliwa kuzindua Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura

Muktasari:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuzindua rasmi Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika katika uwanja wa Mandela, kata ya Pasua mjini Moshi.

Hai. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuzindua rasmi Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakaofanyika katika uwanja wa Mandela, kata ya Pasua mjini Moshi.

Majaliwa aliwasili mkoani hapa leo Julai 18, 2019 saa nne asubuhi na alipokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (Kia) na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Bunge, Ajira na Vijana  Jenista Mhagama akiongozana na viongozi wa mkoa.

Pia, akiwa mkoani hapa atatembelea ujenzi wa mradi wa stendi ya Ngangamfumuni iliyopo Manispaa  ya Moshi.

Julai 19, Majaliwa atapokea taarifa ya mradi wa maji Same, Mwanga-Korogwe (SMK) pamoja na kutembelea  mradi huo.

Julai 20, atazindua treni ya mizigo   katika  reli ya Tanga kilimanjaro.