VIDEO: Mawakala 1000 wa Chadema Arusha mjini waapishwa

VIDEO: Mawakala 1000 wa Chadema Arusha mjini waapishwa

Muktasari:

Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Arusha mjini leo Jumatano Oktoba 21, 2020 kimetinga na mawakala zaidi ya 1,000 kuapishwa wakiongozwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Godbless Lema.

Arusha. Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Arusha mjini leo Jumatano Oktoba 21, 2020 kimetinga na mawakala zaidi ya 1,000 kuapishwa wakiongozwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Godbless Lema.

Mawakala hao ambao wameapishwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha, Dk John Pima walianza kufika shule ya msingi Arusha kuanzia saa moja asubuhi.

Akizungumza wakati anawaapisha mawakala hao, Dk Pima amewataka kuheshimu sheria  na kutotoa siri za matokeo.

Lema akizungumza baada ya kuapishwa amesema wamejipanga kuwa na mawakala katika kituo vyote.

"Hadi sasa katika jimbo la Arusha sijapata malalamiko zoezi linakwenda vizuri,” amesema.

Mgombea udiwani wa Chadema kata ya Revolosi, Ephata Nanyaro amesema katika kata zote 25 kuna wastani wa mawakala 70.

Mgombea udiwani kata ya sokoni (CCM) Michael Kivuyo amesema zoezi la kuapishwa mawakala lilikuwa likiendelea vizuri.

Katika Jimbo la Arusha kuna upinzani mkubwa baina ya wagombea Lema wa CCM na Mrisho Gambo (CCM).