Mbowe wenzake wakutwa na hatia Kisutu

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatia viongozi nane wa Chadema na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dk Vincent Mashinji.
Washtakiwa hao wametiwa hatiani katika mashtaka 12 kati ya 13, yaliyokuwa yanawakabili ikiwemo la uchochezi.
Uamuzi wa kuwatia hatiani, umetolewa leo Jumanne, Machi 10, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama  hiyo, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande  wa mashtaka na ule wa utetezi.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya mahakama kuwatia hatiani washtakiwa hao, ndugu, jamaa na marafiki waliopo ndani ya mahakama hiyo walianza kulia kimya kimya huku wakifuta machozi.
Mbali na Mbowe na Dk Mashinji, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Pia wamo mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko; mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche

Endelea kufuatilia mwananchi kwa habari zaidi