Meli kubwa, ndogo kuanza kutumia bandari mpya Rukwa

Muktasari:

Mradu wa ujenzi wa bandari mpya Kabwe katika Ziwa la Tanganyika, Wilayani Nkasi mkoani Ruvuma umefikia asilimia 85, kukamilika kwake kutaongeza ukubwa wa biashara kiwango cha biashara ya bandari kati ya Tanzania na Congo.

Rukwa. Mradi wa ujenzi bandari mpya ya kabwe ambao unagharimu Sh7.49 bilioni tayari umekamilika kwa asilimia 85, kukamilika kwake kutaziwezesha meli kubwa na ndogo za abiria na mizigo kutia nanga.

Ujenzi huo unaoendelea na ukarabati katika bandari nyingine unatarajia kuongeza ukubwa wa biashara kati ya Tanzania na Congo kupitia bandari zilizopo.

Mkandarasi wa ujenzi huo ambaye ni Sumry's Enterprises Ltd anatarajia kuukabidhi mradi huo Aprili mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi, William Shila amesema leo Ijumaa Desemba 20, 2019 amesema mwenendo wa mradi ni mzuri na unakwenda na muda hivyo utakamilika kwa wakati.

"Tuna changamoto ya mamba na hali ya hewa wakati mwingine mawimbi yanakuwa makali lakini kwa kiwango kikubwa mradi umeleta fursa kwani tumeajiri wazawa wengi na kila mwezi tunatumia zaidi ya Sh30 milioni kwa ajili ya malipo," alisema.

Amesema kigezo kikubwa ni kujua kuogelea na kufanya kazi ndani ya maji.

Mhandisi wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Nyakato Lwamnana anasema mradi wa bandari ya kabwe unahusisha jenzi gati, ofisi, majengo ya abiria pamoja na barabara ya mita 600 ya kuelekea eneo la bandari kati yake mita 150 zikiwa ni za barabara ya zege.

Lwamnana anasema kukamilika kwa mradi huo utakuwa kivutio kikubwa cha biashara katika ya Wilaya ya Nkasi na eneo la Moba nchini Congo.

"Congo wananunua bidhaa nyingi za madukani na vyakula kutoka upande huu wa Tanzania, biashara itaimarisha zaidi baada ya kukamilika kwa gati hili," amesema.

Hivi sasa nchi ya Congo inachangia asilimia 75 ya mizigo yote inayopita kataka bandari za ziwa Tanganyika na kwamwaka jana bandari hizo zilihudumia tani 199,831.