Mfumo kufuatilia miradi ya maendeleo Dar wazinduliwa

Muktasari:

Lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo wa kidijitali ni kutatua changamoto ya kusuasua kwa miradi na kuongeza ufuatiliaji.

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeanzisha mfumo wa kidijitali  kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo.

Mfumo huo umezinduliwa leo Jumatano  Januari 15, 2019 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lengo likiwa ni kutatua changamoto ya kusuasua kwa miradi na kuongeza ufuatiliaji.

Makonda amesema taarifa za miradi yote inayotekelezwa Dar es Salaam zitawafikia viongozi na zitawekwa  wazi kujua kila hatua ya mradi.

“Tumeona kuna shida katika utekelezaji wa miradi  hadi Rais aliliona hilo sasa ni lazima tufanye kitu, ndio maana tumekuja na mfumo huu.”

“Sasa tutajua mradi gani unasimamiwa na nani na umefikia wapi,  kama umekwama nini kimekwamisha na uzembe uko wapi,” amesema Makonda