Mghwira ataka ujenzi wa barabara kuendana na shughuli za uchumi

Thursday October 10 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania,

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania,  Anna Mghwira 

By Florah Temba, Mwananchi [email protected]

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania,  Anna Mghwira amezitaka halmashauri zote za Mkoa huo kuandaa mtandao wa barabara  kwa kuzingatia uimarishaji wa shughuli za kiuchumi maeneo ya vijijini.

Ametoa kauli  hiyo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 wakati akifungua kikao cha kawaida cha bodi ya barabara, kubainisha kuwa  barabara za vijijini zinasahaulika na kuachwa bila kufanyiwa matengenezo.

Amesema kuna umuhimu halmashauri za Wilaya kuhakikisha mtandao wa barabara unazingatia kuimarisha shughuli za uchumi zikiwemo za mashambani na katika migodi.

Amebainisha kuwa barabara zinazounganisha maeneo yenye fursa za uchumi kama masoko, mashamba na biashara nyingine ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha zinafanyiwa matengenezo.

 

 

Advertisement

Advertisement