Mtifuano wa Dk Bashiru, wapinzani D’ Salaam

Muktasari:

Dk Bashiru jana alianza ziara katika baadhi ya majimbo ya mkoa huo huku viongozi wa vyama vya upinzani wakikosoa mienendo wanayokutana nayo ya mikutano yao kuzuiwa mara kwa mara.


Joto la uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 pamoja na uchaguzi mkuu wa mwakani, limeanza kupanda baada ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally na viongozi wa vyama vya wapinzani kuanza kutifuana jijini Dar es Salaam.

Dk Bashiru jana alianza ziara katika baadhi ya majimbo ya mkoa huo huku viongozi wa vyama vya upinzani wakikosoa mienendo wanayokutana nayo ya mikutano yao kuzuiwa mara kwa mara.

Viongozi hao wa vyama vya upinzani wamekwenda mbali zaidi na kudai Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa na kwamba kitendo cha chama tawala pekee kuruhusiwa kufanya mikutano na wao kuzuiwa haina afya kwa mustakabali wa demokrasia nchini.

Dk Bashiru alianza ziara katika Jimbo la Ubungo linaloongozwa na Saed Kubenea (Chadema) na Jimbo la Kibamba la John Mnyika (Chadema) ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa kile alichokisema hivi karibuni kwamba atayatembelea majimbo yote ya jiji hilo kwa lengo la ‘kufunga mitambo’.


KWA HABARI ZAIDI SOMA GAZETI LA MWANANCHI LEO