Mtoto wa Mwanamfalme wa Uingereza atambulishwa kwa Askofu Tutu

Muktasari:

Archie  ambaye ni mtoto wa Mwanamfalme wa Uingereza Harry na Mkewe Meghan wamemtambulisha mtoto wao kwa Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwaza mtoto huyo anaonekana hadharani tangu alipozaliwa miezi minne iliyopita.

Capetown, Afrika Kusini. Mwanamfalme wa Uingereza Harry na Mkewe Meghan (The Duke and Duchess of Sussex) wamemtambulisha mtoto wao Archie aliyezaliwa miezi minne iliyopita kwa Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini.

Hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kufanya safari ya pamoja ya masafa ya mbali, pia ni kwa mara ya kwanza mtoto wao kuonekana hadharani tangu alipozaliwa.

Archie alikuwa akionyesha tabasamu wakati akiwa amebebwa na mama yake na Askofu Tutu.

Askofu Tutu ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobeli na mashuhuri wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi alisema anaona furaha na ni heshima kubwa kwake kukutana na familia hiyo ya kifalme.

Aidha katika mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika taifa hilo la kusini mwa Afrika, The Duke and Duchess of Sussex walizulu maeneo mbalimbali ikiwemo shule, msikiti wa kale na vituo vya misaada kwa watu

Akizungumza katika eneo la rekodi kubwa ya uhalifu, Meghan akiwa na mmewe amesema anapongeza kazi inayofanywa kudhibiti unyanyasaji dhidi ya watoto na wanawake.

Katika eneo hilo walilozulu inaelezwa mwaka uliopita takribani wanawake na 2,700 na watoto 1,000 waliuliwa na wanaume, huku matukio ya ubakaji 100 yakiripotiwa.