Mugabe kuzikwa Septemba 15, viongozi watakiwa kuwahi siku mbili kabla ya mazishi

Monday September 9 2019

Mwili wa Rais mstaafu wa Zimbabwe,  Robert Mugabe, mwananchi habari,Singapore

Robert Mugabe  

By By Elizabeth Joachim, Mwananchi

Mwili wa Rais mstaafu wa Zimbabwe,  Robert Mugabe aliyefariki dunia Septemba 7, 2019 akiwa Singapore utazikwa Septemba 15, 2019 nchini Zimbabwe.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Septemba 9, 2019 huku eneo la atakapozikwa likiwa bado siri.

Mwili wa mwanamapinduzi huyo utawasili Zimbabwe Septemba 11, 2019  na Septemba 14 utapelekwa katika viwanja vya mpira wa miguu vya Harare, huku viongozi mbalimbali wakiombwa kuwasili nchini humo Septemba 13.

Mazishi ya Mugabe yatafanyika Septemba 15, 2019.

Mugabe aliyepigania uhuru wa nchi hiyo hadi ilipopata uhuru April 18, 1980, ameliongoza Taifa hilo kwa miongo mitatu kuanzia mwaka huo hadi alipoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo Novemba 2017.

Mugabe ameacha mke na watoto watatu.

Advertisement

Advertisement