Ndugai awapoza wabunge miradi ya maji, aishauri Serikali

Tuesday September 3 2019Spika wa Bunge la Tanzania,  Job Ndugai

Spika wa Bunge la Tanzania,  Job Ndugai 

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania,  Job Ndugai amesema kero ya kutokamilika kwa miradi ya maji ni ya wabunge wengi  na kuitaka Serikali kushauri namna ya kushughulikia suala hilo kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 11.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumanne Septemba 3, 2019 wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa  Mpwapwa (CCM), George Lubeleje aliyesema  miradi ya maji inachukua hadi miaka minne kukamilika wakati inatumia fedha za ndani.

“Waziri wa maji atoe kauli hapa bungeni kwa nini miradi ya maji inachukua miaka mitano hadi sita haikamiliki naomba mwongozo wako mheshimiwa Spika,” amesema.

Akijibu Ndugai amesema Serikali imelisikia  na watatazama namna  ya kuwashauri, akisisitiza kuwa suala hilo ni kero inayowagusa wabunge wengi.

“Wakati tunaelekea kwenye kimbembe maana bado mikutano mitatu  tu (Kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la 11). Serikali itatushauri namna gani ya kuendana na jambo hili,” amesema Ndugai.

 

Advertisement

Advertisement