Neville aibeba Chelsea, aiponda Liverpool

Saturday September 21 2019
livapic

London, England. Gary Neville amesema atakuwa furaha ikiwa Liverpool itafungw katika mchezo wao dhidi ya Chelsea.

Liverpool kesho itakuwa ugenini  Uwanja wa Stamford Bridge kuikabili Chelsea, katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, alidai atakuwa na furaha Chelsea ikipata pointi tatu, lakini si kwasababu zake binafsi.

Neville alisema sababu ya kutaka Liverpool ifungwe ni kuongeza ushindani kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Alisema msimu uliopita ulikuwa na ushindani wa kuwania taji la Ligi Kuu, hivyo angependa kuona ukitokea tena.

“Sijasema siipendi Chelsea, lakini ni klabu ngumu kuipenda kwa namna inavyocheza na jinsi wachezaji wake walivyo,”alisema Neville.

Advertisement

Kocha huyo wa zamani wa Valencia, alisema mchezo wa leo wa miamba hiyo utakuwa na ushindani, lakini yeye atakuwa upande wa Chelsea.

‘Nilipenda msimu uliopita ulivyokuwa  na msisimko, kila timu ilipambana ikitaka pointi. Ushindani wa aina ile unaifanya ligi kuwa bora zaidi duniani,”alisema Neville.


Advertisement