Advertisement

Profesa Gabagambi afariki dunia

Tuesday October 20 2020
professapic

Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Profesa Damian Gabagambi

Dar es Salaam. Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Profesa Damian Gabagambi amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo Jumanne Oktoba 20, 2020 inaeleza kuwa Gabagambi amefariki leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

“Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Oysterbay. Menejimenti na wafanyakazi wa NDC tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu,” inaeleza taarifa hiyo.

 

Advertisement