Ramaphosa atembelea makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini yaliyopo Tanzania

Rais wa Afrika Kusini, Cyrill Ramaphosa akiangalia makaburi ya mashujaa wapigania uhuru wa nchi hiyo yaliyopo katika eneo iliyokuwa kambi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo, Mazimbu mkoani Morogoro ambapo kwa sasa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), alipotembelea leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Ijumaa Agosti 16, 2019 ametembelea makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo yaliyopo eneo la Mazimbu mkoani Morogoro

Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Ijumaa Agosti 16, 2019 ametembelea makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo yaliyopo eneo la Mazimbu mkoani Morogoro.

Akiwa na mwenyeji wake waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, rais huyo amefika eneo hilo linaloitwa Solomon Malangu, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Ameonyesha nyumba ambayo wapigania uhuru hao walikuwa wanazikwa kijeshi, pia amepanda mti, kuweka shada la maua katika mnara wa mashujaa uliojengwa eneo hilo.

“Eneo hili wamezikwa watu waliokuja kutoka Afrika Kusini na wengine walizaliwa hapa kwa ajili ya kupigania uhuru, tunawashukuru watu wa Morogoro kwa ushirikiano mliowapa walioishi hapa,” amesema Ramaphosa.

Mmoja ya raia wa Afrika Kusini amefika eneo hilo na kuliona kaburi la baba yake na kubainisha kuwa amekuwa akilitafuta kwa miaka 32.