Serikali ya Tanzania yasema mipango yake inatekelezeka

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji.

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa fedha Dk Ashatu Kijaji amesema Tanzania inajiweza kwa kila kitu hivyo mipango yake niko vizuri na inatekelezeka.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imeeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwamba ndio msingi kuwa mipango yake inatekelezwa.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Novemba 11,2019 bungeni mjini Dodoma na naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati akihitimisha mjadala wa  Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti wa mwaka 2020/21.

Dk Kijaji amesema hakuna jambo linaloshindikana huku akitaja ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, mradi wa umeme pamoja na ujenzi wa maboma ya vituo afya na shule.

"Tunaweza kufanya mambo yetu wenyewe hakuna wa kutufanyia, tunaweza kukusanya mapato yetu na kuyapangia matumizi bila shida yoyote, tunajiweza katika mipango," amesema Kijaji.