VIDEO:Fanya haya ukiwa ndani ya gari iliyozama kwenye maji

Thursday October 10 2019

 

By Jafari Juma, Mwananchi

Kutokana na matukio mengi ya magari kusombwa na maji wakati wa mafuriko, nimeona ni vema pia nikaongelea hili suala hapa.

Ni muhimu sana kukumbuka kwamba kitu chochote chenye hewa iliyo-fungwa ndani kama matairi ya gari kitaelea majini.

Hivyo, mara nyingi sana, hata kwenye maji yanayoonekana kuwa na kina kidogo, gari zinakuwa na mwelekeo wa kuelea kwenye maji mengi.

Hii ni kwa gari zote, kubwa na ndogo. Hivyo ni muhimu sana kutoja-ribu kukatisha au kupita barabara ambayo imefurika maji, hasa maji yanayotembea. Suala muhimu la kukumbuka ni kwamba tairi zime-jazwa upepo, hivyo ukipitisha gari kwenye maji gari itakuwa ina mwelekeo wa kuelea, na itahitaji nguvu kidogo sana kuisomba na kuipeleka nje ya barabara.

 


Advertisement

Advertisement