Advertisement

VIDEO:Mawakala wa uchaguzi kuapishwa kwa siku tatu

Wednesday October 21 2020

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuongeza muda wa kuwaapisha mawakala hadi Oktoba 23 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk Wilson Mahera ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Oktoba 21, 2020 uliofikiwa katika kikao kilichowahusisha maofisa wa NEC.

Dk Mahera amesema hatua hiyo imefikiwa kwa kuzingatiwa kuwa baadhi ya maoneo yana changamoto ya kufikika kwa urahisi kwa sababu za kijiografia.

Amesema hali hiyo imesababisha ugumu kwa wasimamizi wa uchaguzi kuweza kuwafikia mawakala hao na kuwaapisha kwa mujibu wa sheria.

Dk Mahera amesema pamoja na kuongezwa muda ni lazima vyama vipeleke orodha ya mawakala na kuwapanga katika vituo pamoja na anuani na namba zao za simu.

Advertisement