Waandamana kupinga marufuku ya kutoa mimba

Saturday October 24 2020
mimbapic

Muandamanaji akiwa ameshikilia bango kupinga uamuzi wa mahakama kuhusu utoaji mimba. AFP

Warsaw, Poland (AFP). Maelfu ya wananchi wa Poland jana Ijumaa Oktoba 23,2020  waliandamana kupinga uamuzi ambao unaweza kuzuia kabisa utoaji mimba katika nchi ambayo ina sheria kali kuliko zote za Umoja wa Ulaya (EU).

Waandamanaji walikuwa katika majiji kadhaa, wakiwa wamechukizwa na uamuzi wa mahakama ya katiba uliotolewa Alhamisi kwamba sheria iliyopo ambayo inaruhusu mimba iliyotungwa vibaya kutolewa, "haiendani" na kulinda maisha.

Uamuzi huo uliibua lawama kutoka kwa makundi ya kutetea haki na nje ya nchi hiyo ambayo wananchi wake wengi ni Wakatoliki.

"Ni vita" au "tunakuja kukupata wewe, wewe katili" linasomeka bango moja lililochorwa picha ya mwanga mwekundu ambao umekuwa alama ya hasira za waandamanaji'.

"Uamuzi wa jana unamaanisha kupiga marufuku kabisa utoaji mimba kwa kuwa asilimia 98 ya watu wanatoa mimba nchini Poland hutokana na kutungwa vibaya kwa mimba," Krystyna Kacpura, kiongozi wa Shirikisho la Wanawake na Uzazzi wa Mpanmgo, aliiambia AFP.

"Ni aibu kwa serikali kwa karibu nusu fa watu wa Poland, wanawake. Hatutasahau hili."

Advertisement
Advertisement